Recent Posts

PropellerAds

Monday, March 14, 2016

Madhara ya pombe kwa mwanamichezo


Mwanamichezo ambaye anashiriki michezo
yupo katika hatari ya kushusha kiwango chake,
endapo atakuwa anaendekeza kunywa pombe
kupitiliza.
Mtakumbuka klabu ya Arsenal iliwahi kumtema
mchezaji wake, Nicolaus Betender kutokana na
kuporomoka kiwango kulikochangiwa kwa kiasi
kikubwa na unywaji pombe uliopitiliza.
Mtu anapokunywa pombe, huingia katika
mfumo wa kusaga chakula na kati ya asilimia
20 hadi 25 ya pombe hiyo hunyonywa haraka na
kuingia katika mzunguko wa damu na kufika
katika ini na huendelea kuvunjwavunjwa.
Mnywaji huanza kuhisi hali ya kulewa pale
pombe inapofika katika ubongo, mwanzoni
unaweza kuhisi kuwa unapata utulivu na
burudani kwa sababu pombe ni kileo inashusha
shinikizo na kupumbaza ubongo.
Kadiri unavyozidi kubugia pombe, ndipo
kiwango cha pombe kinavyozidi kupanda na
hadi kufikia kiwango cha kuleta madhara
mwilini.
Pombe inaweza kumsababishia mwanamichezo
kukosa nguvu, misuli kuuma na kuwa dhaifu,
kuwa mchovu, kushindwa kuwa makini
uwanjani, kukosa utulivu, kichwa kuuma,
kubadilika tabia ikiwamo ukali au ukorofu na
kuongezeka uzito kiholela.
Kawaida Pombe inatumia maji mengi na nishati
nyingi ya mwili ili kuweza kuvunjwa vunjwa,
ndiyo maana mtu hukosa nguvu hapo baadaye
na kupata uchovu mkali.
Vile vile, maji mengi hupotea wakati wa
kunywa pombe kwa njia ya mkojo, hii ni kwa
sababu pombe husisimua homoni inayochochea
figo kuruhusu maji (mkojo) kutoka kwa wingi.
Hivyo hali hii inaweza kumsababishia mtu
kupata upungufu mkali wa maji mwili hivyo,
kumweka mwanamichezo katika hatari ya
misuli kubana au kupata vijeraha katika misuli
wakati wa kucheza.
Pombe inasababisha protini tunayoipata kwa
kula vyakula kutonyonywa katika mfumo wa
chakula. Kukosekana kwa kirutubisho hiki kwa
mwanamichezo misuli yake haitajengeka na
kuimarika.
Pia protini ndiyo inayochangia misuli kujikunja
na kukunjuka, upungufu wa protini
husababisha misuli kutofanya kazi yake kwa
ufanisi hivyo mchezaji hukosa kasi anapokuwa
uwanjani. Pombe inachangia kushusha kiwango
cha homoni ya kiume ijulikanayo kama
testosterone ambayo ndiyo inatuwezesha misuli
kukua na kujikarabati, kwa mwanamichezo
misuli imara ndiyo kila kitu. Unywaji Pombe
uliopitiliza husababisha kukosa hamu ya kula
kutokana na kupoteza vitamini na madini/
chumvichumvi za mwili, kumbuka ukiwa
mwanamichezo kabla na baada ya mechi au
mazoezi makali, unahitaji mlo kwa ajili ya
kupata nguvu. Pombe inaweza kuambatana na
kupata uraibu hivyo kukusababishia uhisi kuwa
bila pombe maisha hayaendi. Ushuari, kwa
mwanamichezo wenye malengo, ni vizuri
kujiepusha na unywaji wa pombe.