Recent Posts

PropellerAds

Thursday, March 31, 2016

Wafadhili wasitisha ufadhili kwa bajeti ya Tanzania

Mataifa 10 ya Magharibi yamesema hayataendelea na
ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.
Baadhi ya nchi hizo ni Sweden na Ireland. Nchi hizo
zinaendelea na msimamo huo ikiwa ni siku chache
baada ya shirika la utoaji misaada la serikali ya
marekani (MCC) kuondoa msaada wake wa dola 472
za ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa Tanzania.
Bodi ya MCC ilisema hatua yake ilitokana na mzozo
kuhusu uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar na utekelezwaji
wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.
Mataifa yaliyositisha ufadhili wao kwa bajeti ya Tanzania
hata hivyo hayajaeleza sababu ya kufanya hivyo.
Ubalozi wa Sweden umethibitisha kwamba taifa hilo
limesitisha ufadhili wake kwa bajeti ya Tanzania, lakini
ukasisitiza kwamba hatua hiyo haihusiani na yaliyojiri
katika uchaguzi wa visiwa vya Zanzibar.
Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC
Uchaguzi wa Zanzibar waikosesha hela Tanzania
"Mwaka uliopita, Sweden ilikuwa moja ya nchi
zilizositisha ufadhili wake kwa bajeti ya Tanzania
kutokana na tuhuma za ufisadi kuhusiana na sekta ya
kawi [na mkataba wetu na serikali ulifika kikomo
mwaka jana],” ubalozi huo umeambia BBC.
“ Sweden inafurahishwa na juhudi za serikali kukabiliana
na ufisadi na iko tayari kuanzisha majadiliano na
serikali ya Tanzania na wafadhili wengine kuhusu
mikakati ya kufadhili bajeti ya Tanzania siku zijazo.”
Ubalozi wa Ireland pia umethibitisha kwamba ni kweli
taifa hilo halifadhili tena bajeti ya Tanzania.
Ufadhili wake wa mwisho ulitolewa mwaka wa kifedha
wa 14/15, malipo ambayo yalifanyika Juni 2015 na
kwa sasa hakuna malipo yaliyoratibiwa ya mwaka wa
kifedha wa 15/16.
"Mpango ulimalizika Juni 2015 na hakuna mipango
mingine ya kutoa ufadhili kwa bajeti (ya Tanzania),”
ubalozi wa nchi hiyo umesema.
Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea
msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua ya nchi hizo
ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.