Afisa mwengine wa ngazi ya juu katika jeshi la Burundi
ameuwawa usiku wa jana katika hali ya kutatanisha
katikati mwa jiji la Bujumbura.
Meja Didier Mihimpundu ameuawa saa chache baada ya
kuuawa kwa kamanda wa kambi moja muhimu mjini
Bujumbura Kanali Darius Ikurakure akiwa kwenye makao
makuu ya jeshi mjini Bujumbura .
Kamanda wa kambi ya Bujumbura Kanali Darius
Ikurakure ameuawa
Meja Didier Muhimpundu aliuawa karibu saa mbili ya
usiku .
Polisi wanasema alipokea simu na kuondoka ndani ya
baa moja mjini Bujumbura kabla ya kufyatuliwaa risasi.
Hadi sasa waliomuuwa afisa huyo aliyekuwa msimamizi
wa idara ya afya ya jeshi , hawajafahamika kwa mujibu
wa naibu msemaji wa polisi Moise Nkurunziza.
'' Meja Muhimupundu alipigiwa simu na mtu akiwa
katika baa, halafu alipotoka kutaka kukutana na mtu
huyo, wakampiga risasi, na akafariki papo hapo,''
''Uchunguzi umeanzishwa kujua vema watu hao
waliofanya ukatili huo , na hivo wafikishwe mbele ya
vyombo vya sheria kuadhibiwa. alisema Nkurunziza.
Saa moja kabla ya Meja Muhimpundu kuuwawa,
kulisikika milio ya risasi Kaskazini mwa jiji katika mtaa
wa Carama .
Wakaazi sehemu hiyo wanathibitisha polisi mmoja
aliuwawa katika ufyatulianaji huo wa risasi.
Hata hivo polisi imekanusha taarifa hizo na kutaja kuwa
alitekwa.
'' Polisi huyo alitekwa na watu waliokuwa katika gari la
watu binafsi, ambao walikuwa wamevalia sare za
kijesh.''
''Taarifa za kuuliwa kwake si sahihi hazina ukweli
maana haijaonekana maiti yake'' alisema msemaji wa
polisi Nkurunziza.
Awali jana mchana aliuwawa Kamanda wa kambi moja
muhimu ya kijeshi hapa nchini Luteni Kanali Darius
Ikurakure akiwa ndani ya makao makuu ya jeshi hapa
mjini Bujumbura.
Mauaji hayo ya mfululizo yameanza kutafsiriwa kama
ulipizanaji kisasi katika jeshi lenye mchanganyiko wa
makabila na kutishia uwiano wa vikosi vya ulinzi.
Msemaji wa Jeshi Clement Cimana .ameonya kuhusu hali
hiyo'' Makao Makuu ya jeshi yanalaani vikati ukatili
wowote wa aina hii,uongozi wa jeshi unawatolea wito
wanajeshi popote walipo kubaki wanashikamana na
kuwaepuka watu wanaojaribu kuwagawanya kwa lengo la
kusambaratisha jeshi la Burundi.''
Katika kipindi cha miezi minane , maafisa wakuu jeshini
wasiopungua watano wameuawa katika jiji la Bujumbura,
lakini mauaji ya sasa yameibuka baada ya siku kadhaa
za utulivu nchini
Simba SC kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation wamerejesha kwa Jamii
kabla ya mchezo wao na Bravos
-
Kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika
wa Simba SC dhidi ya Bravos ya Angola utakaochezwa Novemba 27, Simba SC kwa
k...
1 hour ago