Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, March 23, 2016

Mshukiwa wa mashambulio ya Brussels ‘atambuliwa’

Mshukiwa aliyekuwa akisakwa sana kuhusiana na
mashambulio ya Brussels ametambuliwa na maafisa wa
usalama, vyombo vya habari Ubelgiji vimeripoti.
Baadhi ya vyombo vya habari limetaja jina lake kuwa
Najim Laachraoui.
Wadadisi wanasema Laachraoui anaaminika kuwa
mtaalamu wa kuunda mabomu.
Alionekana kwenye picha ya kamera za usalama uwanja
wa ndege akiwa pamoja na washukiwa wawili ambao
inadaiwa walijilipua wakati uwanja wa ndege wa
Zaventem.
Alikuwa tayari anatafutwa na polisi kuhusiana na
mashambulio ya Paris mwaka jana.
Ripoti za kukamatwa kwake bado hazijathibitishwa na
maafisa wa usalama.
Taarifa za awali zilikuwa zimewatambua washukiwa
walioonekana naye kwenye uwanja wa ndege kuwa ndugu
wawili, Brahim na Khalid El Bakraoui.
Watu 34 walifariki na zaidi ya 250 kujeruhiwa kwenye
mashambulio mawili yaliyotokea katika uwanja huo wa
ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek.
Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza
mashambulio hayo.
Bendera zinapepea nusu mlingoti nchini Ubelgiji. Taifa
hilo limetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.