Wanachama 89 wa kundi la Kiislamu la Boko Haram
nchini Nigeria wamehukumiwa kifo nchini Cameroon
baada ya kupatikana na makosa kujihusisha na ugaidi.
Wanachama hao wamehukumiwa na mahakama ya kijeshi
kwa mchango wao katika mashambulio kadha eneo la
kaskazini mwa Cameroon linalopakana na Nigeria, kwa
mujibu wa idhaa ya BBC Hausa.
Eneo hilo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na
wanamgambo wa Boko Haram.
Waliohukumiwa ni sehemu ya wanachama 850
wanaozuiliwa nchini Cameroon kwa kudaiwa kuhusika na
mashambulio ya kundi hilo la Kiislamu.
Hii ni mara ya kwanza kwa watu kuhukumiwa kifo chini
ya sheria mpya za kukabiliana na ugaidi zilizopitishwa
mwaka 2014.
Sheria hiyo hupendekeza kifo kwa wanaopatikana na
makosa ya ugaidi.
Watu 22 walihukumiwa kifo mwaka 2013.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 7, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 7,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
2 hours ago