Recent Posts

PropellerAds

Thursday, March 17, 2016

AU kutuma waangalizi wa uchaguzi Zanzibar

Tume ya Umoja wa Afrika imetangaza kwamba
itawatuma waangalizi wa uchaguzi wa marudio visiwani
Zanzibar ambao utafanyika Jumapili.
Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Nkosazana Dlamini Zuma
ameidhinishwa kutumwa kwa wataalamu sita wa kufuatilia
uchaguzi huo wa tarehe 20 Machi.
Vyama sita vya upinzani, kikiwemo Chama cha
Wananchi (CUF) vimetangaza kwamba vitasusia
uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unatokana na kufutwa kwa matokeo ya
uchaguzi wa urais na wawakilishi uliofanyika tarehe 25
Oktoba mwaka jana.
Chama cha CUF kilipinga hatua ya kufutwa kwa
matokeo hayo .
Mgombea wake wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad,
alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo wa mwaka jana.
CUF kususia marudio ya uchaguzi Zanzibar
Sababu 8 za kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar
Juhudi za kutumia mazungumzo kutafutia ufumbuzi mzozo
wa kisiasa uliotokana na kufutwa kwa matokeo hayo
hazikufua dafu.
Kupitia taarifa, AU imesema: “Kuambatana na wajibu
wake, Tume ya Umoja wa Ulaya itatuma ujumbe wa
wataalamu Zanzibar kuhakikisha kwamba uchaguzi wa
marudio ni wa amani, wa kuaminika na unatimiza
viwango vya AU vya uchaguzi wa kidemokrasia.”
Ujumbe huo utakuwa visiwani Zanzibar kati ya tarehe
17 na 25 Machi.