Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, March 22, 2016

Burundi: Mkuu wa jeshi auawa kambini

Afisa mmoja muandamizi wa jeshi la Burundi ameuwawa
leo ndani ya makao makuu ya jeshi la Burundi.
Kanali Darius Ikurakure alikuwa Kamanda wa kambi ya
kijeshi ya Muzinga, nje kidogo ya jiji la Bujumbura.
Kambi ya Muzinda iko kilomita 30 kutoka mji mkuu wa
Bujumbura.
Kanali Ikurakure alikua msatari wa mbele katika
harakati za kuzima maandamano na ghasia zilizotokea
baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania
muhula wa tatu mamlakani.
Duru kutoka kwa jeshi la burundi zinasema kuwa kanali
huyo alipigwa risasi na mwanajeshi mwenza.