Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa amri kwa
wanajeshi walioko Syria kurejea nyumbani mara moja
kwa sababu tayari wametekeleza asilimia kubwa ya
malengo yao.
Akizungumza katika ikulu ya Kremlin Putin, alisema
''Tayari tumeshakamilisha asilimia kubwa ya madhumuni
yetu nchini Syria kwa hivyo kuanzia jumanne (kesho)
ningependa asilimia kubwa ya jeshi letu kurejea
nyumbani.'' alisema bwana Putin.
Tangazo hilo lake limewaacha wachanganuzi wengi
wamepigwa na mshangao kwani hakukuwa na dalili
zozote za kuwepo kwa tukio kama hilo.
Aidha Putin ametangaza hilo katika siku ambayo
mazungumzo ya amani yameanza upya mjini Geneva
Uswisi.
Urusi ni mshirika wa karibu sana wa rais wa Syria
Bashar al-Assad.
Ikulu ya Kremlin inasema kuwa rais Bashar al-Assad
alifahamishwa kuhusu hatua hiyo.
Itakumbukwa kuwa kuingia kwa majeshi ya Urusi katika
vita vya Syria vilibadili kabisa taswira ya vita hivyo.
Kwa wakati huo waasi walionekana kuwa walikuwa
wanaelekea kuishinda nguvu jeshi la Syria kinyume na
hali ilivyo sasa ambapo majeshi watiifu kwa rais Assad
wameanza hata kuteka maeneo yaliyokuwa chini ya
waasi.
Rais Putin hata hivyo amesema kuwa kambi ya kijeshi
ya Hmeimim na bandari ya Tartus itasalia chini ya jeshi
la Urusi.
Huku akisisitiza kuwa zitalindwa ''kwa hewa ardhini na
hata baharini''
Simba SC kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation wamerejesha kwa Jamii
kabla ya mchezo wao na Bravos
-
Kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika
wa Simba SC dhidi ya Bravos ya Angola utakaochezwa Novemba 27, Simba SC kwa
k...
30 minutes ago