Wakuu katika serikali ya Jamhuri ya Congo
wameamrisha kampuni mbili kuu za simu, kufunga
mawasiliano yote ya simu, wakati wa uchaguzi wa urais
hapo kesho.
Wizara ya mashauri ya ndani ya nchi ilisema imefunga
mawasiliano kwa sababu za usalama.
Mgombea wa upinzani, John Marie Michel Mokoko,
alisema amepokea amri ya kwenda polisi, na alisema
hiyo ni hatua ya kumzuia yeye katika kugombea
uchaguzi.
Wagombea wanane wanampinga Rais Denis Sassou
Nguesso.
Katiba ilibadilishwa mwaka jana, kumruhusu agombee
tena uongozi.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 7, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 7,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
2 hours ago