Aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Luis Inacio Lula da Silva,
amekubali cheo cha uwaziri ndani ya serikali ya Dilma
Rousseff.
Wanachama wa chama cha wafanyikazi wamesema kuwa
uteuzi huo utaupa nguvu utawala wake unaolegea.Akiwa
waziri Lula atakuwa na haki ya kinga.
Wiki iliopita waendesha mashtaka walitaka akamatwe
kutokana na uchunguzi wa ulanguzi wa fedha wa jumba
moja la kifahari lililopo katika ufukwe wa bahari.
Rais huyo wa zamani aliye na umaarufu mkubwa
amekana kufanya makosa yoyote na kusema kuwa madai
hayo yanashinikizwa kisiasa.
Akiwa waziri Lula anawezi kushtakiwa na mahakama ya
juu pekee na hivyobasi kumuondoa mbele ya meno ya
jaji aliye kusini mwa mji wa Curitiba ambaye
anahusishwa na uchunguzi huo.
Lula alizuiliwa kwa mda mapema mwezi huu baada ya
uchunguzi kusema kuwa kuna ushahidi alipokea faida
katika mpango ulioshirikisha kampuni ya mafuta ya
Petrobras.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 7, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 7,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
2 hours ago