Recent Posts

PropellerAds

Monday, March 21, 2016

Magufuli ahakiki bunduki zake mbili

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa bunduki
zake mbili aina ya shortgun na pistol na zikahakikiwa
nyumbani kwake ikulu jijini Dar es salaam.
Kiongozi huyo ndiye mtu kwanza kutekeleza agizo la
mkuu wa mkoa wa Dar es salaam la kuhakiki silaha,
kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Uhakiki wa silaha hizo umefanywa na maafisa wa Jeshi
la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda
Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Rais
Magufuli ametoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha
nchini humo kuhakikisha zinahakikiwa.
Aidha, amelitaka jeshi la polisi kuongeza juhudi za
kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya
uhalifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
"Ni aibu kumuona askari polisi mwenye silaha
ananyang'anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni
aibu, mpaka jambazi akunyang'anye silaha na wewe una
silaha?" amesema Dkt Magufuli.