Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, March 22, 2016

Watu 31 wauawa katika mashambulio Brussels

Watu 31 wamefariki baada ya mashambulio kutekelezwa
katika uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha
treni cha Maelbeek mjini Brussels.
Waziri wa afya wa Ubelgiji amesema watu 11 walifariki
na wengine 81 kujeruhiwa baada ya milipuko miwili
kutokea uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo ya
mji wa Brussels.
Meya wa Brussels amesema watu 20 walifariki
Maelbeek.
Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza
mashambulio hayo
Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Hollande amelaani
mashambulio hayo mjini Brussels na kusema ni kama
mashambulio yaliyolenga bara lote la Ulaya.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema hatua
zaidi zimechukuliwa kuimarisha usalama mpakani.
Kwa Picha: Mashambulio ya Brussels
Mshukiwa wa Paris alitaka kujilipua
Mchezaji wa DR Congo anusurika Brussels
Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa
kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya
mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.
Abdeslam alikamatwa Ijumaa katika mtaa mmoja wa
Brussels.
Uwanja wa ndege wa Zaventem unapatikana kilomita 11
kaskazini mashariki mwa Brussels na ulihudumia abiria
zaidi ya 23 milioni mwaka jana.