Recent Posts

PropellerAds

Friday, March 25, 2016

Korea Kaskazini yafanya zoezi la kushambulia makao ya rais

Korea Kaskazini imesema kuwa imetekeleza mazoezi ya
kuyashambulia makaazi ya rais wa Korea Kusini.
Zoezi hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong-
un,kulingana na chombo cha habari cha KCNA ambaye
alilitaka jeshi kujiandaaa kuivamia na kuiharibu serikali
ya kusini.
Ni hatua ya hivi karibuni ya ishara za hasira za
Pyongyang.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameliagiza jeshi
lake kuwa katika hali ya tahadhari.
Lakini alisema siku ya Alhamisi kwamba uchochezi
utasababisha maafa makubwa kwa serikali na uongozi wa
Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini imekuwa ikijibu hatua ya Umoja wa
Mataifa ya kuiwekea vikwazo kufuatia majaribio ya
makombora yake ya masafa marefu ya kinyuklia.
Pyongyang vile vile imekasirishwa na mazoezi ya pamoja
kati ya serikali ya Korea Kusini na Marekani kusini mwa
mpaka wake.
Kama inavyojulikana kwa vitisho vyake ,ripoti hiyo
iliotolewa na KCNA ilitishia kuilipua nyumba hiyo ya
rais wa Korea Kusini inayojuliakana kama Blue House
hadi kuwa jivu.
Makombora yalirushwa kama umeme na kuanguka katika
maeneo yanayolengwa ikiwemo nyumba hiyo ya rais wa
Korea Kusini.
Haijulikani ni lini zoezi hilo lilifanywa,lakini ripoti hiyo
ilionya mwisho mbaya wa rais Park.
Makaazi hayo ya Blue House yalishambuliwa na
makomando wa Korea Kaskazini mwaka 1968.
Hatahivyo jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa rais Park
Chung-hee halikufanikiwa,raia saba wa Korea Kusini
pamoja na makomando hao 31 kutoka Korea Kaskazini
waliuawa.