Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, March 16, 2016

Obama aongezea vikwazo Korea kaskazin

Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha vikwazo
vipya dhidi ya Korea Kaskazini baada ya taifa hilo
kufanyia majaribio silaha za nyuklia na makombora hivi
majuzi.
Msemaji wa ikulu ya White House amesema Marekani
na jamii ya kimataifa hawatavumilia “shughuli haramu
za nyuklia” zinazotekelezwa na Korea Kaskazini.
Awali, ikulu ya White House iliishutumu Korea Kaskazini
ikisema inawatumia raia wa Marekani kama rahani
katika juhudi za kuendeleza ajenda yake ya kisiasa.
Korea Kaskazini yaamrisha majaribo zaidi ya
mabomu
Korea Kaskazini yajibu vikwazo vya UN
Hii ni baada ya Korea Kaskazini kumhukumu mwanafunzi
Mmarekani kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu jela
kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola.
Bw Otto Warmbier, mwenye umri wa miaka 21, alikiri
kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akikaa
pamoja na kundi jingine la watalii mjini Pyongyang.
Marekani imeitaka Korea Kaskazini kumwachilia huru
mwanafunzi huyo mara moja.