Recent Posts

PropellerAds

Sunday, March 20, 2016

Ladislas Ntaganzwa asafirishwa Rwanda

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda,
amesafirishwa kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo
kwenda nchini Rwanda ambapo atakabiliwa na
mashtaka.
Kulingana na wakuu wa mashitaka nchini
Rwanda,wanamtuhumu Ladislas Ntaganzwa kuongoza
magenge ya wakereketwa wa kihutu waliofanya
mashambulio dhidi ya watutsi,ugavi wa silaha na
kuwabaka wanawake.
Kesi dhidi yake itasikilizwa nchini Rwanda baada ya
mahakama ya kimataifa ya ICTR kufunga milango mwaka
2015. Kesi nyingine zitaendeshwa na taasisi iliyochukua
nafasi ya mahakama hiyo.
Marekani ambayo ilitangaza zawadi ya dola milioni tano
kwa mtu ambaye atasaidia akamatwe, ilimtaja kama
moja wa wachochezi wakubwa wa mauaji hayo katika
eneo la kusini la Butare.
Ladislas Ntaganzwa alikuwa amewekewa waranti wa
kukamatwa na mahakama ya uhalifu nchini Rwanda
ambayo ilimaliza shughuli zake mwezi Desemba mwaka
2015. Maelfu ya watu waliuawa nchini Rwanda mwaka
1994 wengi wao wakiwa ni watutsi.
Alikimbia Rwanda mwaka 1994 mara tu baada ya
mauaji ya kimbari na kuchukua hifadhi katika Jamuhuri
ya kidemokrasia ya Congo.
Alikuwa kwenye orodha ya watuhumiwa wakuu wa mauaji
ya kimbari ambao bado wanasakwa kwa udi na uvumba
dunia nzima na ambao serikali ya Marekani iliweka
zawadi kwa yeyote atakayewakamata ama kutoa taarifa
zitakazopelekea wao kukamatwa.