Recent Posts

PropellerAds

Thursday, March 17, 2016

Mwanafunzi aliyemtishia Trump kuondoka Marekani

Mwanafunzi wa urubani kutoka Misri aliyeandika kwenye
Facebook kwamba ulimwengu unaweza kumshukuru sana
akimuua Donald Trump ameamua kuondoka Marekani kwa
hiari.
Emadeldin Elsayed, 23, hakufunguliwa mashtaka yoyote
ya uhalifu lakini maafisa wa Marekani walitaka
afurushwe, wakili wake Hani Bushra amesema.
Maafisa wa hamiaji wamesema anaweza kuruhusiwa
arejee nyumbani salama na kwa hiari mradi tu awe
ameongoka kufikia tarehe 5 Julai.
Kwa sasa Elsayed anazuiliawa katika jela moja jimbo la
California baada ya viza yake kufutiliwa mbali.
Bw Bushra alisema Jumatatu kwamba Elsayed anazuiliwa
kinyume cha sheria.
“Anazuiliwa, nafikiri, kwa sababu yeye ni Mwislamu na
mtu kutoka Mashariki ya Kati,” Bw Bushra aliambia
shirika la habari la AP.
Mwanafunzi wa Misri kufurushwa US baada ya
kumtishia Trump
Trump ashutumiwa kwa kupanga kufurusha wahamiaji
Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
“Kijana huyu ataanza kutumiwa katika mabango ya
kuichukia Marekani.”
Bw Elsayed alihojiwa na makachero wa Marekani
mapema Februari baada yake kupakia picha ya Bw
Trump kwenye Facebook na kuandika kwamba ako radhi
kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kumuua bilionea
huyo na kwamba ulimwengu unaweza kumshukuru kwa
hilo, Bw Bushra alisema.
Bw Elsayed alikuwa awali amesema kwamba hakukusudia
kumdhuru yeyote.
Alisema aliandika hayo kutokana na matamshi ya Bw
Trump kuhusu Waislamu.
Bw Trump alikuwa mwisho mwa mwaka jana
amependekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.