Recent Posts

PropellerAds

Friday, March 25, 2016

Kiongozi wa IS auwawa Syria

Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika itifaki ya kundi la
wapiganaji la Islamic State ameuawa katika oparesheni
iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu,
vyombo vya habari vya Marekani vimesema.
Maafisa wa ulinzi wameliambia shirika la habari la NBC
kwamba Abdul Rahman Mustafa al- Qaduli,raia wa Iraq
anayejulikana kama Hajji Iman aliuwawa katika uvamizi
mwezi huu.
Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash
Carter alitarajiwa kuthibitisha kifo cha mwana jihad
huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo.
Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba
kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli.
Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa
mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu
mwaka 2014.
Alijiunga na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya
uongozi wa marehemu Abu Musab al-Zarqawi akihudumu
kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul
kulingana na Marekani.
Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema
mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.