Recent Posts

PropellerAds

Monday, March 14, 2016

Ujenzi wa bomba la mafuta Tanga kuanza karibuni

Kampuni inayotarajiwa kufanikisha ujenzi wa bomba la
mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda
imesema iko tayari kuanza ujenzi huo.
Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki
Bw Javier Rielo amemwambia Rais wa Tanzania John
Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi huo haraka
iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo
zipo.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa
kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka
ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na
ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Magufuli na Museveni wajadili bomba la mafuta
Bw Javier, akikutana na Rais Magufuli ikulu ya Dar es
salaam, amesema kampuni yake inatarajia kutumia dola
za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari
zimeshaandaliwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Rais Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha
mchakato wa kuanza kwa mradi, na kupendekeza muda
wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo
upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana
mapema.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo,
Tanzania pia inatarajia kunufaika zaidi na bomba hilo,
kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea
katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania.
Amesema zikikamilika kwa mafanikio, inatarajiwa bomba
hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
Makubaliano ya kujengwa kwa bomba hilo yaliafikiwa
wakati wa mkutano kati ya Rais Magufuli na Rais wa
Uganda Yoweri Museveni mapema mwezi huu.