Kumekuwa na mapigano kati ya wanajeshi wa kenya na
wanamgambo wa al-Shabaab katika eneo la Lower Juba
nchini Somalia.
Kuna ripoti za kukanganya kuhusu maafa.
Wanajeshi wa Kenya wanasema kuwa walivisiwa lakini
wakafanikiwa kuwaua wanamgabo 21 licha ya wao
kupoteza wanajeshi wawili.
Al-Shabab nao wanadai kuwa waliwaua wanajeshi 20
wa Kenya wakawakamata wawili na kuharibu magari yao
sita.
Mapigano hayo yalitokea kwenye barabara inayoelekea
mji wa Afmadow ambapo wanajeshi wa kenya waliwaua
wanamgambo 19 wa al-Shabab siku ya Jumatano.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha
kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini
ke...
5 weeks ago