Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, March 30, 2016

Marekani yalalamikia UN kuhusu Iran

Marekani na washirika wake kutoka Ulaya
wameulalamikia Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ya Iran
ya kufanyia majaribio makombora ya masafa marefu.
Mataifa hayo yamesema majaribio hayo yanakiuka azimio
la Umoja wa Mataifa.
Azimio hilo ambalo liliidhinisha mkataba wa nyuklia
baina ya UN na Iran liliitaka Iran kutofanyia majaribio
makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba
silaha za nyuklia.
Trump aahidi kuvunja mkataba wa nyuklia
Iran yaanza kutekeleza mkataba wa nyuklia
Kwenye barua, iliyopatikana na Reuters, maafisa wa
Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wameeleza
wasiwasi wao kuhusiana na madai ya Iran kwamba
makombora hayo yameungwa mahususi kuwa tishio kwa
Israel.
Mataifa hayo manne yameliomba Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa kujadili hatua zinazofaa kuchukuliwa.
Hata hivyo, hayakusema waziwazi kwamba majaribio
hayo ya makombora yanakiuka azimio la Umoja wa
Mataifa kuhusu Iran.
Makombora hayo yalikuwa yameandikwa kauli mbiu:
“Israel sharti iangamizwe”, ikiwa imeandikwa kwa
Kiyahudi.