Recent Posts

PropellerAds

Friday, March 25, 2016

Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu

Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameosha
miguu ya wahamiaji waislamu mjini Rome katika tukio la
unyenyekevu linaloambatana na itikadi ya kuanza kwa
msimu wa Pasaka.
Papa Francis alitembela makao ya wahamiaji, mjini
Roma na kuendesha misa ya kuanza kwa msimu wa
pasaka.
Ziara yake katika kituo hicho cha kutathmini uhalali wa
wahamiaji cha (Castelnuovo di Porto), inawadia huku
uhasama na taharuki ikienea kote barani ulaya kuhusiana
na kuwepo kwa wahamiaji waislamu hususan kufuatia
mauaji ya Paris mwezi Novemba na ya hivi punde huko
Brussels Ubelgiji.
Papa Francis alikashifu mauaji yaliyotokea Ufaransa na
Ubelgiji akisema kuwa hizo ni njama za watu wenye kiu
cha kumwaga damu ya binadamu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alilaumu
mtazamo wa watuhumiwa hao kuhusu maafa
waliyosababisha.
Aidha papa mtakatifu aliwashauri watu wa dini tofauti
duniani kuishi kwa amani.
''Haijalishi iwapo tunaimani tofauti la muhimu kwetu
sote ni tuishi kwa amani sisi ni ndugu alisema papa
mtakatifu.