Simba aliyetoka katika mbuga ya taifa ya wanyama ya
Nairobi amemshambulia mzee mmoja jijini humo mapema
asubuhi.
Simba huyo alitoka mbugani na kuonekana karibu na
eneo la City Cabanas, katika ya Mombasa Road.
Afisa wa mawasiliano wa Shirika la Huduma kwa
Wanyamapori (KWS) Bw Paul Udoto ameambia BBC
kwamba mzee aliyejeruhiwa ni wa umri wa miaka 63
na amepewa matibabu ya dharura katika uwanja wa
ndege wa Jomo Kenyatta kisha akakimbizwa hospitalini
kwa matibabu kamili.
Hata hivyo, Bw Udoto amesema mzee huyo hayuko
hatarini.
Kwa mujibu wa afisa huyo, simba huyo huenda alikerwa
na kelele za magari yaliyokuwa yakipita.
Vikosi vitatu vya maafisa wa KWS vilitumwa kumdhibiti
na kwa mujibu wa Bw Udoto, simba huyo anaelekezwa
ndani kwenye mbuga.
Maafisa wanaendelea kushika doria kubaini iwapo kuna
simba wengine walitoka mbugani.
Visa vya simba kutoka mbugani vimekuwa vikiripotiwa
siku za karibuni. Mwezi mmoja uliopita, simba wanne
waliingia maeneo ya makazi eneo la Langata.
Wiki mbili zilizopita, simba wawili walidaiwa kuonekana
karibu na barabara ya Ngong.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 5, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 5,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini ...
5 hours ago