Gavana wa Istanbul, Uturuki, anasema watu wanne
wameuwawa katika mripuko wa bomu kufuatia shambulio
la kujitolea mhanga katikati ya mji.
Watu wengine kama 20 wamejeruhiwa.
Picha za televisheni zimeonesha magari ya kubeba
wagonjwa, yakielekea eneo la mashambulio, ambalo sasa
limetengwa na polisi.
Jumapili iliyopita, shambulio jengine lilifanywa katika mji
mkuu wa Uturuki, Ankara, na kuuwa watu 37.
Chama cha waopiganaji wa KiKurd, TAK, kilisema
kilihusika na shambulio hilo.
Wanafunzi Kapeta,Kiwira warithishwa ari ya utunzaji mazingira
-
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kwa kushirikiana na Shirika la
Utangazaji la Tanzania (TBC), wameendesha zoezi la upandaji miti katika
Shule ya msi...
8 hours ago