Mgombea urais wa chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump amebadili msimamo wake muda
mfupi baada ya kusema wanawake wanaotoa mimba
wanafaa kuadhibiwa, utoaji mimba ukiharamishwa.
Alikuwa ametoa tamko lake katika hafla iliyopeperushwa
moja kwa moja na kituo cha runinga cha MSNBC.
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali.
Lakini muda muda mfupi baadaye, alibadili msimamo
wake na kusema ni wahudumu wa afya wanaosaidia
wanawake kutoa mimba pekee wanaofaa kuadhibiwa.
Lakini hata baada ya kusema hivyo, alijitetea na
kuongeza kuwa: “Msimamo wangu haujabadilika.”
Mgombea huyo anayeongoza katika chama cha
Republican anaunga mkono kupigwa marufuku kwa utoaji
mimba, lakini kwa kutegemea hali.
Utoaji mimba umekuwa halali nchini Marekani tangu
1973 kufuatia uamuzi wa kihistoria wa Mahakama ya
Juu nchini humo.
Trump aahidi kuvunja mkataba wa nyuklia
Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump
Ni kupitia Mahakama Kuu pekee au marekebisho ya
katiba ambapo uamuzi huo katika kesi ya Roe v Wade
unaweza kubatilishwa na uavyaji mimba kuharamishwa.
Bw Trump, ambaye wakati mmoja alikuwa mfuasi wa
chama cha Democratic, ameshutumiwa awali kwa kutetea
haki za wanawake kutoa mimba.
Msimamo rasmi wa chama cha Republican ni kwamba
utoaji mimba unafaa kuwa haramu.
Wanasiasawahafidhina na wanaharakati wanaochukulia
utoaji mimba kuwa sawa na mauaji, hata hivyo, mara
nyingi hukwepa kuwekea lawama wanawake wanaotoa
mimba na badala yake kuwalaumu wanaowasaidia
wanawake kutoa mimba.
Lengo kuu la hili huwa kuvutia wananchi ambao kimsingi
hawawezi wakafurahia kuwaona wanawake wengi
walioshika mimba kimakosa wakifungwa jela kwa kutoa
mimba.
Viongozi wa chama cha Republican wameeleza wasiwasi
wao kuhusu kuidhinishwa kwa Bw Trump kuwa mgombea
wa chama hicho katika uchaguzi mkuu Novemba, hasa
kwa sababu kura za maoni zinaonesha hapendwi sana
na wapiga kura wa kike.
Bw Trump ameshutumiwa kwa kuwadhalilisha wanawake
wakiwemo aliyekuwa mgombea urais Carly Fiorina na
mtangazaji wa runinga Megyn Kelly.
Meneja wake, Corey Lewandowski, alikamatwa Jumanne
akituhumiwa kumshambulia mwanahabari wa kike.
Bw Trump amemtetea Bw Lewandowski akisema
hakutenda kosa lolote.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 7, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 7,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
2 hours ago