Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, March 23, 2016

Al Shabab yapiga marufuku bidhaa za Uturuki

Kundi la wanamgambo wa Al Shabab limepiga marufuku
uuzaji na ununuzi wa bidhaa zilizoundwa Uturuki nchini
Somalia.
Al-Shabab imewaarifu wafanyibiashara katika majimbo
ya Kusini mwa Somalia na maeneo ya Lower Shabelle
kuwa bidhaa zinazotokea Uturuku ni haramu.
Jarida linalochapishwa kwenye tovuti ya Falaar inasema
kuwa wale watakaokiuka amri hiyo ''watachomwa moto
wakiwa hai''
Wafanyibiashara katika maeneo yaliyoathirika tayari
wamelalamika kuwa amri hiyo itawaathiri vibaya.
Al-Shabab inasema kuwa imechukua hatua hiyo kwani
Uturuki inasaidia mahasidi wao serikali ya Somalia.
Hii sio mara ya kwanza kwa Al shabab kuilenga
Uturuki.
Awali Al Shabab ilikuwa imelalamika kuwa bidhaa
zinazotokea Uturuki zinatokomeza uchumi wa Somalia.
Wafanyibiashara kutoka Uturuki wamewekeza katika
biashara nyingi nchini Somalia na haswa Mogadishu