Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, March 16, 2016

Korea Kaskazini yatishia kuishambulia Marekani

Korea Kaskazini imetishia kutekeleza mashambulio ya
nyuklia dhidi ya Korea Kusini na Marekani iwapo nchi
hizo mbili zitaendelea na mazoezi ya pamoja ya kijeshi.
Mazoezi hayo, ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka
huu yatashirikisha wanajeshi 300,000.
Serikali ya Korea Kaskazini imetoa taarifa ya ikitishia
kutekeleza “shambulio la nyuklia kwa ajili ya haki”.
Ni kawaida kwa Pyongyang kutoa vitisho vya aina hiyo
na wataalamu wanatilia shaka uwezo wa Korea
Kaskazini kuwa na makombora ya nyuklia.
Hisia hupanda kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini
na Marekani kila mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi
yanapofanyika.
Pyongyang hutazama mazoezi hayo kama mazoezi ya
kujiandaa kuivamia.
Korea Kaskazini kuweka tayari silaha za nyuklia
Mhubiri wa Canada afungwa maisha Korea Kaskazini
Korea Kaskazini yatangaza kamanda mpya wa jeshi
Mwaka uliopita, Korea Kaskazini ilitishia kugeuza
Washington kuwa “bahari ya moto”.
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imeionya Pyongyang
dhidi ya “hatua za haraka zisizo za busara ambazo
zinaweza zikailetea maangamizi”.
Mazoezi ya mwaka huu, yanayoshirikisha wanajeshi
300,000 wa Korea Kusini na 15,000 wa Marekani,
ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika.
Yanaandaliwa siku chache tu baada ya Umoja wa
Mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea
Kaskazini kutokana na hatua yake ya kufanyia majaribio
bomu la nyuklia na kufyatua makombora.
Korea Kaskazini ilijibu vikwazo hivyo kwa kutangaza
itaweka tayari silaha zake za nyuklia na pia ikavyatua
makombora ya masafa mafupi baharini.