Kiongozi wa upinzani ambaye pia ni mwekezaji, Patrick
Talon anatarajiwa kushinda uchaguzi wa Urais nchini
Benin, baada ya kumshinda Waziri Mkuu Lionel Zinsou.
Matokeo kamili yanatarajiwa kutolewa baadaye leo,
Waziri Mkuu Zinsou amempongeza mpinzani wake.
Bwana Talon anachukua hatamu ya uongozi kutoka kwa
Rais Thomas Boni Yayi ambaye amemaliza mihula
miwili.
Katika visiwa vya Cape Verde, chama cha upinzani
MPD kimepata viti vingi zaidi vya ubunge. Visiwa hivyo
vitafanya Uchaguzi wa Urais baadaye mwaka huu.
Katika nchi za Niger na Congo- Brazaville wapiga kura
wanasuburi matokeo ya uchaguzu mkuu.
Nchini Senegal matokeo ya kura ya maoni yanatolewa
kuhusu marekebisho ya katiba ikiwemo kupunguza muhula
wa Rais kutoka miaka saba hadi mitano.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 7, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 7,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
2 hours ago