Recent Posts

PropellerAds

Thursday, March 31, 2016

Aliyewakinga wakristo kutoka kwa al shabab atuzwa

Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo
wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali
ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa
wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa
kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.
Rais Kenyatta alihutubia taifa
Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa
heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The
Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.
Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa
likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi
kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al
shabab.
Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu
na wale wasio waislamu.
Al Shabaab: Wanawake waislamu waliwafunika Hijab
wakristo
Waislamu waokoa wakristo waliotekwa na al Shabab
Hapo ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu
waliponga'amua nia ya wapiganaji hao ilikuwa ni kuua
wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga abiria wakristo
miongoni mwao ilikuokoa maisha yao.
Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya
kukataa kugawanywa kwa makundi.
Kwa bahati mbata Mwalimu Farah alifariki mwezi
Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa
takriban mwezi mmoja.
Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa
wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na
magaidi wa Al Shabab.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya
Makkah kutekwa.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al
Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28
ambao hawakuwa waislamu.
Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili
mwaka uliopita lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika
chuo kikuu cha Garissa.