08:50 Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed
amezungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake
katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja.
Mwanzo amezungumzia hatua ya Chama cha Wananchi
(CUF) kususia uchaguzi huo.
Kuhusu amani na utulivu, amesema anaamini kutakuwa
na utulivu visiwani.
Hii hapa video yake akizungumza:
08:13 Kumbuka, Chama cha Wananchi (CUF)
kilitangaza kwamba hakitashiriki uchaguzi wa marudio
unaoendelea leo. Chama hicho kinaamini kilishinda
uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na
mgombea wake Maalim Seif Hamad anafaa kutangazwa
mshindi.
Tume ya uchaguzi Zanzibar hata hivyo ilitangazwa
kwamba hakuna aliyejiondoa rasmi kutoka kwa uchaguzi
wa leo.
Lubuva: Magufuli hafai kuingilia kati Zanzibar
08:00 Maafisa wa usalama wakishika doria mjini Chake
kisiwani Pemba.
07:50 Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es
Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.
Hapa chini ni tangazo la kuwapasha wateja wa Azam
Sealink kwamba hakutakuwa na safari za meli kuanzia
tarehe 18 hadi 22 Machi kutokana na uchaguzi
unaoendelea Zanzibar.
Licha ya kukatizwa kwa safari, badi wapo watu
waliojitokeza wakitarajia kusafiri. Wengi wa waliofika ni
wageni kutoka Ulaya ambao hawakuwa na habari.
07:44 Usalama umeimarishwa visiwani. Hapa chini ni
maafisa wa usalama wakiwa na mbwa wa kunusa kabla
ya Dkt Shein kupiga kura yake katika kituo cha Bungi,
Unguja.
07:42 Baadhi ya wapiga kura wakitafuta majina yao
kituoni Madungu Chake-Chake, kisiwani Pemba.
07:30 Mwanamke akipakwa wino kwenye kidole chake
baada ya kupiga kura kituo cha Madungu Chake-Chake,
Pemba.
Baadaye, atabasamu baada kutoka nje ya ukumbi.
07:20 Hii hapa ni picha nyingine ya Dkt Ali Shein,
mgombea urais wa CCM baada yake kupiga kura
Unguja.
07:05 Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali
Mohammed Shein amepiga kura yake katika kituo cha
Bungi, Kibera katika kisiwa cha Unguja.
07:00 Vituo vingi vya kupigia kura vimefunguliwa.
06:50 Maafisa wa uchaguzi wanajiandaa kufungua vituo.
Vituo vinafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa
kumi alasiri.
06:40 Wapiga kura kituo cha Bungi, Unguja wasubiri
kituo kifunguliwe.
06:35 Katika vituo vingi, wapiga kura hajawafika.
Lakini maafisa wa tume tayari wamo vituoni pamoja na
maafisa wa usalama. Hata ni kituo cha Madungu
Chake-Chake, Pemba.
06:30 Hujambo! Wapiga kura visiwani Zanzibar
wanashiriki uchaguzi wa marudio leo baada ya matokeo
ya uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba mwaka jana kufutwa
na tume ya uchaguzi. Chama cha CUF kinasusia
uchaguzi huo.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi
huo.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 7, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 7,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
2 hours ago