Kulala kwa masaa mengi au kwa muda mfupi vinaweza kuchangia mtu kunenepa kupita kiasi
Utafiti
umegundua kuwa usingizi usio mzuri unaweka mtu kwenye hatari ya
kunenepa kupita kiasi kwa watu walio na maumbile ya kunenepa.Hali hiyo ilishuhudiwa licha ya mtu kupata mankuli yanayostahili na kuwa na afya nzuri.
Watafiti waliangalia athari za kulala chini ya saa 7 kwa usiku na kulala masaa mengi zaidi, kama masaa tisa na hata kulala saa za mchana.
Waligundua kuwa watu wenye miili ya kunenepa , kulala kwa muda mfupi au masaa mengi, vyote vinachangia mtu kunenepa, ikilinganishwa na watu wanaolala muda unaotakikana wa kati ya masaa saba na nane.
Wanaolala masaa mengi na walio na miili ya kunenepa wanaweza kuwa na uzito wa kilo 4 zaidi, huku wale wanaolala muda mfupi wakipata uzito wa kilo 2 zaidi.
Takwimu hizo zilionyesha kuwa walio na jeni za kunenepa na wanaolala saa chache au saa nyingi, ambao hulala mchana na wakati wa mapumziko kazini, walionekana kuwa na athari kwa uzito wa miili yao.