Recent Posts

PropellerAds

Thursday, March 2, 2017

Mwanasheria mkuu US atakiwa kujiuzulu kwa kuwasiliana na Urusi

Mwansheria mkuu Jeff Sessions kulia ametakiwa kujiuzulu kwa kuwasiliana na Urusi
Mwanasheria mkuu nchini Marekani jenerali Jeff Sessions alikutana na balozi wa Urusi wakati wa uchaguzi licha ya kuthibitisha kuwa hakufanya mawasiliano yoyote na Urusi.
Idara ya haki ilithibitisha kuwa alikutana na Sergei Kislyak mnamo mwezi Julai na Septemba mwaka uliopita ikiwa ni miongoni mwa majukumu yake katika kamati ya bunge la seneti ya huduma za usalama.
Bw Session alisema kuwa matamshi yake yalifananishwa na jukumu lake katika kampeni ya rais Trump.
Madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani yamemkabili rais Trump.
Sergei Kislyak wa Urusi

Idara ya ujasusi inaamini kwamba udukuzi unaodaiwa kufanywa na Urusi dhidi ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton ulifanywa ukiwa na lengo la kumsaidia bw Trump kumshinda Clinton.
Mshauri wa maswala ya usalama wa rais Trump Michael Flynn alifutwa kazi mwezi uliopita baada ya kuidanganya ikulu kuhusu matamshi yake na bw Kislyak, kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi

Related Posts:

  • MAGAZETI YA LEO MARCH 31 Read More
  • HOTUBA YA TRUMP YATUMIKA KATIKA FILAMUWazalishaji wa filamu moja nchini Mexico kuhusu wahamiaji wanaojaribu kuingia nchini Marekani wametoa kipande kidogo cha filamu hiyo ambacho kinatumia hotuba ya bwana Donald Trump kupitisha ujumbe wa filamu hiyo kwamba maneno… Read More
  • Trump ayumbayumba kuhusu utoaji mimbaMgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amebadili msimamo wake muda mfupi baada ya kusema wanawake wanaotoa mimba wanafaa kuadhibiwa, utoaji mimba ukiharamishwa. Alikuwa ametoa tamko lake katika haf… Read More
  • Chama chatisha kumuondoa Zuma madarakaniChama cha Democtratic Alliance nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka katiba. Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma alikataa kutii … Read More
  • Daraja laporomoka na kuwaua 10 IndiaTakriban watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya daraja moja la juu lililokuwa likijengwa kuporomoka kwenye mji wa mashariki mwa India wa Kolkata Ripoti zingine zinasema kuwa karibu watu 150 huenda wamekwama ch… Read More