Recent Posts

PropellerAds

Thursday, March 2, 2017

Utafiti: Unene unasababisha aina 11 za saratani

Mtoto anayeugua ugonjwa wa kunenepa kupitia kiaisi
Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kwamba wamethibitisha kuwepo kwa uhusiano mkubwa kati ya kunenepa na aina kumi na moja za saratani.
Watafiti wamebaini kwamba unene unasababisha saratani kadhaa ikiwemo saratani ya tumbo, ini, matiti, utumbo na kizazi
Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Imperial mjini London, wanasema, kando na kuepuka uvutaji sigara, kutunza uzani unaozingatia afya bora, ndio njia moja muhimu inayopunguza uwezekano wa kuugua saratani.
Shirika la afya duniani linasema asilimia 40 ya watu wazima kote duniani ni wanene.