Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua mama Salma Kikwete kuwa
Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.Mama Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Salma ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa na ushawihi mkubwa sana wa kisiasa ndani ya chama chake.