Recent Posts

PropellerAds

Thursday, March 2, 2017

Sasa ni marufuku wanafunzi kupigwa viboko Zimbabwe

Ni marufuku kuwachapa viboko wanafunzi na watoto nyumbani

Mahakama ya Zimbabwe imepiga marufuku adhabu ya kuwachapa watoto shuleni na hata nyumbani .
Uamuzi huo unajiri baada ya mzazi mmoja kulalamika kwamba mwanawe katika darasa la kwanza alikuwa na majeraha mabaya baada ya kuchapwa na mwalimu.
Linah Pfungwah alisema kuwa mwanawe aliadhibiwa kwa kushindwa kutoa kitabu chake kwa wazazi kutiwa saini kama thibitisho la kwamba alifanya kazi yake ya shule.
Mahakama ya katiba inatarajiwa kuthibitisha uamuzi huo.

Wanafunzi wapata afueni baada ya mahakama kuamuru kwamba hawafai kuchapwa
Mwandishi wa BBC Shingai Nyoka katika mji mkuu wa Harare anasema kuwa iwapo uamuzi huo utathibitishwa utabadilisha vile wazazi wanavyowaadhibu wanawao kwa karne kadhaa katika taifa hilo la Afrika ya kusini.
Baadhi ya wazazi wanakosoa uamuzi huo, huku makundi ya haki za kibinaadamu yakisema ulitarajiwa

Related Posts:

  • Trump alegeza msimamo kuhusu WaislamuMgombea Urais wa Republican anaonekana kulegeza msimamo kuhusiana na pendekezo lake tata la kuwazuia Waislamu kuingia Marekani. Katika mahojiano na kituo cha television cha Fox News, Donald Trump akijibu kauli ya meya mpya wa… Read More
  • 50 wafariki kwenye mafuriko EthiopiaTakriban watu 50 wamefariki kufautia mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliosababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo Ethiopia. Taifa hilo la upembe wa Afrika linakabiliwana ukame mbaya kuwahi kushuhudiwa katika miaka… Read More
  • Kongamano la uchumi kufanyika Rwanda Kongamano la 26 la uchumi duniani linaanza leo mjini Kigali Rwanda. Hii ni mara ya kwanza kongamano hilo kuandaliwa Rwanda na mara yake ya pili kufanyika afrika mashariki. Kongamano hilo litakalowaleta pamoja marais wa mat… Read More
  • Besigye akamatwa kwa 'kujiapisha' UgandaTaharuki imetanda nchini Uganda baada ya kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye, ''kujiapishwa kama rais'' siku moja tu kabla ya kuapishwa rasmi kwa rais Yoweri Museveni . Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa kizuizi … Read More
  • MAGAZETI YA LEO MEI 12 Read More