Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe
ameenda Singapore kufanya vipimo vya Afya yake, siku chache baada ya
sherehe ya kufikisha miaka 93.
Mugabe amekua dhaifu zaidi, na sasa anapata shida hata kutembea wakati wa matukio mbalimbali ya kitaifa.Msemaji wa rais huyo alisema kuwa vipimo hivyo ni vya mara kwa mara na Rais anatarajiwa kurejea nchini Zimbabwe wiki ijayo.
Mugabe ni kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani, aliingia madarakani mnamo mwaka 1980.