Inawezekana una ndoto au mipango ya kuishi maisha ya namna fulani ambayo
unayoyataka. Je, kitu cha kujiuliza, ulishawahi kujua utawezaje kushi
maisha hayo unayoyataka?
Je, ni mikakati ipi ambayo umeweka hadi uweze kufikia hatua ya kuweza
kutengeneza maisha unayoyataka? Kwa kawaida bila hata kuumiza kichwa,
yapo mambo ya kuzingatia ili yakusaidie kuishi maisha unayoyataka.
Haya ni mambo ya msingi sana ambayo ukizingatia yatakusaidia uweze
kutengeneza maisha bora unayohitaji. Unajiuliza ki-vipi, hapa nikiwa na
maana maisha ya ndoto zako, ikiwa lakini utachukua hatua.
Ni mambo gani ambayo unatakiwa kufanya ili kutengeneza maisha ya
mafanikio unayoyataka? Hebu fuatana nami katika makala haya ili tuweze
kujifunza kwa pamoja.
1. Tambua kitu unachokitaka.
Ikiwa haujui kile unachotaka vizuri kwenye maisha yako, usije ukashangaa
ukaendelea kuwa mtu wa kutokuwa na mafanikio karibu kila siku. Kabla
hujapata kitu chochote kwenye haya maisha lazima uje ni kipi unataka.
Watu wengi wanakwama sana kwenye maisha kwa sababu ya kutokujua vizuri
wanachotaka. Chukua muda wako kidogo ulionao na kisha kitambue kile
unachokitaka kwenye maisha yako.
2. Tengeneza mfumo wa kufikia hicho unachokitaka.
Kwa kuwa umeshakijua hicho unachokitaka katika maisha yako, sasa hapa
unatakiwa kutengeneza mfumo wa kuhakikisha unakikamilisha kitu hicho.
Unatengeezaje huo mfumo? Ni kwa kufanya kila siku.
Acha kusimamishwa na kitu chochote. Weka nguvu za uzingativu na fanya
kila siku mpaka malengo yako yatimie. Ikiwa utafanya kila siku, uwe na
uhakika baada ya muda utafikia kile unachokitaka.
3. Weka juhudi sana.
Wakati unapokuwa umejiwekea mikakati ya kudfika kule unakotaka kufika
kuna ni rahii tu kujikta unashindwa kufanikisha adhima hiyo ikiwa
huataweka juhudu sana.
Unatakiwa uweke juhudi kuhakikisha mpaka unafanikiwa. Hakuna kulala
katika hilo jitahidi sana ufanye kila linawezekana mpaka kuona kila kitu
kinakaa sawa.
4. Weka nguvu za uzingativu kwa hicho unachokifanya.
Usijiruhusu ukawa mtu wa tamaa, wakati upo kwenye harakati za
kutengeneza maisha unayoyataka wewe. Kati ya kitu kinachowaangusha watu
ni pamoja na tamaa ya kutaka kufanya mambo mengi kwa pamoja.
Ni muhimu nguvu zako ukaziweka sehemu moja. Hata ikitokea jambo zuri
vipi, kipindi ambacho unatengeneza maisha unayoyataka, ukishaweka nguvu
ya uzingativu usilifanye jambo hilo. Kitu cha msingi ujifunze kutulia
ili kufikia mafanikio yako.
5. Jifunze kila siku juu ya kitu hicho.
Njia ya kufikia mafanikio mara nyingi ni njia ambayo haijanyooka kabisa
kama baadhi wanavyofikiri. Zipo changamoto nyingi zinazojitokeza. Kila
zinapotokea changamoto hizo amua kujifunza na kujirekebisha kwa kufanya
upya kila siku
Pale unapokutana na changamoto za aina yoyote ile hutakiwi kukata tamaa
na kutaka kurudi nyuma. Kitu cha muhimu ni kujifunza na kufanya hadi
uone umeweza kufikia lengo la kuishi maisha unayotaka.
Unatakiwa uamua kujifunza juu ya kitu ambacho umeamua kukifanya mpaka
uwe mtaalamu kabisa tena uliyebobea. Kwa hali, hiyo itakusaidia sana
kuweza kuishi maisha unayoyataka.
Mwisho, mtu kuishi maisha anayoyata sio ajali wala bahati. Unaweza
ukaishi maisha unayoyataka ikiwa utatengeneza mfumo huo na kuzingatia
mambo haya muhimu kama tulivyoyaangalia kwenye makala haya.