Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, February 22, 2017

Mbona bado kuna njaa duniani?

Wanawake wakisubiri huduma ya afya jimbo la Unity Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa umetangaza njaa sehemu kadha nchini Sudan Kusini, ambayo ni ya kwanza kutangazwa popote pale duniani katika kipindi cha miaka sita.
Pia kuna onyo la kutokea njaa kaskazini mashariki mwa Nigeia, Somalia na Yemen. Lakini ni kwa nini bado kuna njaa, na ni kitu gani kinastahili kufanywa.
Ni kipi kinaendelea nchini Sudan Kusini?
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa watu 10,000 wanakumbwa na njaa nchini Sudan Kusini na wengine milioni moja wanatajwa kuwa walio kwenye hatari ya kukumbwa na njaa.
Kwa ujumla Umoja wa mataiafa unasema kuwa watu milioni 4.9 au asiimia 40 ya watu wote nchini Sudan Kusini wanahitaji chakula cha dharura.
Chanzo kikuu cha njaa ni mzozo. Nchi hiyo imekumbwa na vita tangu mwaka 2013 ambapo zaidi ya watu milioni 3 wamelazimika kukimbia makwao.
Uzalishaji wa mazao umeathiriwa pakubwa na mzozo hata katika maeneo ambayo yamekuwa yakizalisha mazao mengi baada ya mzozo wa viongozi wa kisababisha kung'angania madaraka pamoja na mali asili miongoni mwa makabila.
Ugavi wa chakula Somalia

Tangazo hilo la njaa ni kumaanisha nini?

Njaa inaweza kutangazwa tu wakati idadi ya vifo na viwango vya utapiamlo vinafikia kiwango fulani, kwa mfano:
  • Ikiwa takriban asilimia 20 ya familia zinakumbwa na uhaba mkubwa wa chakula.
  • Viwango vya utapiamlo vinazidi asilimia 30.
  • Na vifo vinazidi zaidi ya watu 2 kwa siku kati ya watu 10,000.
  • Sehemu zinazokuwa na uhaba wa chakula
    Njaa za awali ni pamoja na kusini mwa Somalia mwaka 2011, ya kuisni mwa Sudan mwaka 2008, ya Gode eneo a Kisomalia nchini Ethiopia ya mwaka 2000, Kore Kaskazini mwaka 1996, Somalia kati ya mwaka 1991 na 1992 na Ethiopia kati ya mwaka 1984 na 1985.

    Ni kipi kinaweza kufanywa Sudan Kusini?

    Ni vitu viwili vinaweza kufanywa ili kukabiliana hali hiyo: misaada zaidi ya kibinadau na kutoa fursa ya kufikiwa kwa maeneo yaliyoathirika zaidi
     Watu wengi nchini Sudan Kusini wanaishi kwenye kambi
    Baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa serikali ya Rais Salva Kiir imekuwa ikizuia chakua cha msaada kuenda maeneo mengine. Imeripotiwa kuwa misafara ya misaada na maghala yamekuwa yakishambuliwa.
    Licha ya serikali kukana madai hayo, Rais Kiir kwa sasa ameahidi kuwa misaada yote ya kibinadamu itawafikia watu wanaohitaji kote nchini .

    Mbona kuna uhaba wa chakula maeneo mengini?

    Chanzo kikuu ni mizozo.
    Yemen, kaskazini mashariki mwa Nigeria na Somalia ni sehemu ambapo mapigano yamevuruga vibaya amani na maisha ya kawaida.
    Nchini Yemen mzozo umevutia mataifa jirani na kusababisha uharibifu mkubwa na kuzorota kwa uchumi.
    Nigeria na Somalia zimekumbwa na makundi ya kigaidi hali ambayo imesababisha kuhama kwa watu wengi, kuvuruwa kwa sekta ya kilimo na shughuli zingine kama biashara.
    Watu nchini Yemen wamekumbwa na ukosefu wa maji Ugaidi kaskaziniamashariki mwa Nigeia umesababisha njaa