Recent Posts

PropellerAds

Saturday, February 18, 2017

''Mugabe anaweza kupigiwa kura akiwa maiti''

Grace Mugabe na mumewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.
Bwana Mugabe, ambaye atakuwa na umri wa miaka 93 mnamo Jumanne, ametangaza mara kadhaa kuwa atagombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Grace Mugabe ana miaka 40 mchanga kwa mumewe.
Aliambia mkutano wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa hata mumewe akifariki, bado jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura.
Alisema watu wa Zimbabwe wanampenda Rais wao sana, hivi kwamba wangempigia kura hata akiwa maiti.
Robert Mugabe
Bi Mugabe amekuwa mkosoaji mkuu wa wakosoaji wa mumewe na kwa wale walio na tamaa ya kumrithi.
Inadhaniwa kuwa alikuwa mstari wa mbele wa kumwachisha kazi aliyekuwa makamu wa rais, Joice Mujuru mwaka 2014.
Bwana Mugabe, ambeye siku hizi haonekani sana hadharani, ametawala Zimbabwe tangu taifa hilo kuwa huru miaka 37 iliyopita.


Related Posts:

  • Kwa nini raia wa Afrika Kusini huchoma shule? Awali iliropotiwa kuwa Shule nane kaskazini mwa Afrika Kusini zilichomwa na waandamanaji. Maandamano nchini Afrika Kusini yana historia ya kubadilika na kuwa ghasia,ikianzia miaka ya nyuma ya utawala wa wakoloni ambapo wak… Read More
  • Justin Bieber ashtakiwa kwa kuvunja simu Mwanamuziki Justin Bieber ameshtakiwa kwa dola milioni 100,000 kwa madai kwamba alivunja simu. Nyota huyo ametuhumiwa kuivunja simu ya Robert Earl Morgan baada ya kujaribu kumrekodi Bieber wakati alipokuwa akinywa pombeKI… Read More
  • Donald Trump azidi kupetaJohn Kasich amejitoa kwenye kinyanganyiro cha mchujo wa kugombea urais katika chama cha Republican na kumuacha Donald Trump kama mgombea wa pekee. Bw Kasich alitoa tangazo hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari nyumbani… Read More
  • Hali ya hatari yatangazwa CanadaGavana wa jimbo la Alberta nchini Canada ametangaza hali ya hatari wakati moto mkubwa wa msituni unapoteketeza maeneo ya mji wa Fort McMurray.Maafisa wanasema kuwa nyumba 1600 na majengo mengine yameharibiwa na moto huo amb… Read More
  • Chama tawala Uturuki kuchagua kiongoziRipoti kutoka nchini Uturuki zinasema kuwa chama tawala cha PKK kitakutana baadaye mwezi huu kumchagua kiongozi mpya kufuatia wiki kadha za tofauti kati ya viongozi wawili wakuu wa chama hicho. Mkuu wa chama waziri mkuu Ahm… Read More