Recent Posts

PropellerAds

Thursday, February 2, 2017

Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi afariki dunia

Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi,
amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji
akiwa na umri wa miaka 84.
Tshisekedi alikwenda mjini Brussels
mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya
matibabu.
DR Congo: Tshisekedi asafirishwa
Ubelgiji kwa matibabu
Tshisekedi: Tutamuonyesha 'kadi
nyekundu' rais Kabila
Utata DRC; wapinzani wadai ratiba ya
uchaguzi wa mwaka huu
Watu 20 wauawa katika maandamano
DR Congo
Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa
wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa
mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.
Alisimama kidete katika utawala wa
aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais
Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake
ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya
kupinduliwa.
Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa
Rais Laurent Kabila, ambae aliingia
madarakani mnamo mwaka 1997, na
mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi
sasa ndio anatawala nchi hiyo.