Ni Kitu gani unachotaka kufanya katika maisha yako? Je unaota ndoto gani
juu ya maisha yako? Je wewe ni mzuri katika eneo gani? Yaani unacho
kipaji gani?
Katika umri wa utoto kila mmoja wetu aliwahi kuigiza
kuhusu jambo fulani, wapo waliowahi kuigiza kuwa ni madaktari, madereva,
wanasiasa, wasanii waigizaji katika filamu na kadhalika na kadhalika.
Wengi
wetu pia tuna ndoto fulani juu ya maisha yetu, ndoto ambazo wakati
mwingine huziona kana kwamba ndivyo maisha yetu yatakavyo kuwa huko
mbele ya safari.
Hapa ningeomba kutahadharisha kwamba kama ndoto zako
zilikuwa hasi na zilikuwa zimejaa maumivu na kukatishwa tamaa au hofu
za kushindwa katika kufikia malengo yako hayo, basi ujue kwamba hayo
ndiyo mavuno ya aidha ulichokuwa nacho leo au utakachovuna kesho
ukubwani.
Mara nyingi inashauriwa na wataalamu wa elimu hii ya utambuzi kuwa ndoto zetu zinatakiwa ziwe ni chanya na za kutupa nafuu.
Kwani ndoto ulizokuwa nazo utotoni au ulizonazo leo inawezekana ikawa ndio matokeo ya shughuli unayofanya leo.
Kama
ulikuwa na malengo tofauti na unachokifanya leo, kwa maana ya kwamba
unachokifanya leo si kile ulichokuwa umekusudia kuwa ndio malengo yako
ya kuwepo hapa duniani basi huajachelewa, unao uwezo wa kuibadilisha
hali hiyo kwa jinsi utakavyopenda.
Kimsingi haitakiwi maisha
yakuendeshe, bali uyaendeshe, kwani wewe ndio mwenye mamlaka ya
kujichagulia maisha uyatakayo na sio maisha yakuchagulie yanavyotaka.
Hebu chunguza mawazo yako ya kina ujue ni kitu gani unachowaza ndani
yako, najua sio jambo rahisi sana kutokana na mazoea, lakini ukiamua
unaweza kabisa ukajua mawazo yaliyo ndani yako na hapo ndipo utakapo
gundua siri kubwa iliyoko katika maisha yako.
Kwa sababu, naamini utagundua kwamba maisha uliyonayo sasa ni matoeo ya kile unachokiwaza na unachokiamini.
Kama
ukigundua kuwa mawazo yako yamejaa majuto na maumivu ya matukio ya jana
na hofu za kesho, basi yakupasa ubadilishe mfumo wako wa kufikiri, na
kuanza kuwaza yale yanayokupa furaha na amani.
Kataa kabisa
mawazo ya kukatisha tamaa na jaribu kuwaepuka marafiki wenye mawazo
yenye kukatisha tamaa kwani hao ndio maadui wakubwa wa kukukwamisha
kufikia malengo yako.
Katika miongoni mwa makala zake kwenye Gazeti
la Jitambue, hayati Munga Tehenan, Mtaaluma wa Elimu hii ya utambuzi
aliwahi kuandika kuhusiana na nguvu ya mawazo pamoja na subira,
aliandika hivi:
“Wakati inawezekana ukawa na hamu ya kuona
malengo yako yanatimia mara moja, ukweli ni kwamba hamu yako ya kuleta
mabadiliko ya haraka yaweza kukuletea madhara zaidi kuliko faida.
Kwa nini? Kwa sababu unakosa subira na hivyo unafanya mambo yako kinyume
na utaratibu wa maumbile. Ukosefu wa subira hutuma ujumbe hasi kwenye
mawazo yako ya kina na wakati huohuo unakuwa unafanya mambo kwa
kupingana na kanuni ya maumbile. Kwa kufanya hivyo hutumii kile
kinachofahamika kama nguvu ya subira. Hii nguvu ya subira yaweza
kupatikana kwa hatua mbali mbali zikiongozwa na kufikiri kwako.
Wakati
unapokosa subira katika kupata mafanikio, unachofanya ni kuisukuma
nafsi yako mbali zaidi kutoka kwenye mafanikio. Wengi wetu hutaka vitu
tunavyoamua kuvipata tuvipate hapo hapo, na pale tunapoamua kubadilika
ama kuboresha hali zetu, tunataka mabadiliko hayo yatokee mara moja ili
mtu aweze kufurahia maisha yetu mapya na kuanza kufurahiya mafanikio.
Lakini
sisi ni sehemu ya maumbile na maumbile hayabadili vitu mara moja.
Mchakato unaweza kuanza mara moja lakini mabadiliko kamili hayawezi
kutokea mara moja.
Kwa vile sisi ni sehemu ya maumbile, ni lazima tufanye kazi kama maumbile yanavyotaka na kwa kufuata taratibu zake.
Linapokuja
suala la kufikia malengo yako, mawazo yako ya kina kama yalivyo
maumbile yanatakiwa kufanya kazi kwa kupitia mchakato na kukuruhusu
kwenda kwa hatua kuelekea kwenye mafanikio ya malengo yako.”
Kwa
maelezo hayo tumeona kuwa maisha ni malengo na malengo ndio mafanikio,
lakini la msingi tusije tukajiumiza kwa kutaka malengo hayo yatokee mara
moja, kuwaza hivyo ni kujiumiza kihisia na kuisababishia miili yetu
maumivu na hivyo kuwa mibovu kiafya.
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
2 hours ago