Recent Posts

PropellerAds

Thursday, February 16, 2017

Watu zaidi wakamatwa kufuatia kifo cha Kim Jong-nam

Washukiwa wawili zaidi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong-nam, ambaye ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un nchini Malaysia.
Mshukiwa mmoja mwanamke raia wa Indonesia na mwanamume raia wa Malaysia ambaye anakisiwa kuwa mpenzi wake wote walikamatwa leo Alhamisi.
Mwanamke mmoja maabye alikuwa na hati ya kusafiri ya Vietnam naye amekamatwa.
Kifo cha Kim: Mwanamke akamatwa Malaysia
Je nani ni muuaji wa Kim Jong Nam?
Kim alifariki siku ya Jumatatau kutokana na kile kinachaoimiw akuwa aliwekeka simu wakati akisubiri kuabiri ndeg mjini Kuala Lumpur.
Polisi wanasema kuwa wamemaliza kuufanyia uchunguzi mwili wake Kim licha ya matokeo kutotangazwa
Washukiwa hao wawili wa wamezuiwa rumande kwa siku saba.
Kuna uvumi unaoenea kuwa Korea Kaskazini ilihusika na mauaji hao.
Picha moja kutoka kwa kamera za usalama ambayo imepepeshwa nchini Korea Kusini na Malaysia, inaonyesha mwanamke mwenye fulana nyeupe yenye jina "LOL".
Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu
Inaaminiwa kuwa Kim alishambuliwa kwenye ukumbi wa kuabiri ndege kwenye uwanja wa ndege na wanawake wawili waliotumia aina fulani ya kemikali
Leo Alhamisi Korea Kaskazini inasherehekea kile kinachotajwa kuwa miaka 75 ya kuzaliwa kwa Kim Jong-il, mareheu kiongozi wa zamani na baba wa Kim Jong-nam na Kim Jong-un.