Recent Posts

PropellerAds

Monday, February 13, 2017

Mkalimani ‘feki’ aliyedaiwa kumpotosha mtali kwa tafsiri aomba radhi Tanzania

Mkalimani akamatwa Tanzania kwa kutafsiri visivyo matamshi ya mtalii

Mkalimani anayedaiwa kutafsiri maneno yasiyo sahihi kutoka kwa mmoja wa watalii aliyetembea hifadhi ya Ngorongoro, hatimaye ameibuka na kuomba radhi kutokana na video hiyo iliyosambaa kwa madai kuwa alikuwa katika mazingira ya kufanya utani.
Awali mkalimani huyo anayeitwa Simon Sirikwa aliwekwa chini ya ulinzi kutokana kile kilichokuwakinatafsiriwa kudaiwa kuwa kilikuwa kinapotosha uhalisia wa maneno yaliyokuwa yakizungumzwa na mtalii aliyekuwa akisifia kile alichokiona baada ya kutembelea eneo hilo la utalii.
Hata hivyo katika video mpya aliyoitoa akiwa na mtalii yule yule aliyeonekana katika video ya kwanza, amesikika akizungumza kwa lugha ya Kiswahili akiomba radhi kwa kile alichokuwa amezungumza kwenye video ya awali.
"Kama mlivyoona video yangu niliyopitisha mimi ni tour guide kwa zaidi ya miaka kumi sasa, siwezi kuichafua hii nchi hata kidogo, hata aliyetoa hiyo video kwenye Facebook, kwenda kwenye Whatsapp na kuisambaza kwenye makundi ya kijamii atakuwa amekosea," amesema Sirikwa.
"Lakini ilikuwa ni comedy, ilikuwa ni utani, na najua kuna watu wamekwazika, ila naomba samahani kwa waliokwazika, ila kwa mafansi wangu, wafuasi wangu endeleeni kupata burudani, ila mfahamu sijafanya hichi kitu kwa serious wala sikuwa na makusudio yoyote mabaya, asanteni."
Baadhi ya watu wanaomfahamu Sirikwa walipohojiwa na BBC wamemuelezea alivyo mtu wa utani na kwamba anajulikana kwa jina la utani kama Mpondamali.
Haijabainika iwapo Sirikwa aliachiliwa huru bila masharti au aliachiliwa huru kwa dhamana.

Cheetahs
Mwanamke mtalii kwenye video hiyo ya pili anasikika akisema: "Hamjambo tena, Sehemu ya pili ya video yetu. Tunacheza tu. Simon alikuwa anafanya ucheshi tu na tulikuwa tunafanya utani tu kidogo kwenye Facebook.
Ijumaa, kamanda wa polisi wa kanda hiyo Jaffari Mohammed aliambia BBC kwamba mwelekezi huyo alikuwa "amempotosha" mtalii huyo na kwamba polisi walikuwa wakifanya uchunguzi kubaini iwapo alisambaza video hiyo mitandao ya kijamii kinyume na sheria za uhalifu wa kimitandao.
Sheria hiyo inatoa faini ya kuanzia $1,300 (£1,000) na kifungo cha kuanzia miezi mitatu jela kwa anayepatikana na kosa la kuchapisha habari za uongo, za kuhadaa au za kupotosha kwa kutumia kompyuta.
Sheria hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2015.
Mwelekezi huyo alikamatwa kwa azigo la Waziri wa Utalii Jumanne Maghembe.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam anasema kuwa huenda waziri alihisi kuwa mkalimani huyo alikuwa akimsuta mtalii au alikuwa akimuiga Rais John Magufuli.
Kwenye video hiyo asili, mtalii anasema:
 Watalii wengi huzuru Tanzania kuona wanyamapori
"Hi. Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri. watu ni wazui na wenye urafiki. Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa, Ardhi ni nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia nja wakati mna maua nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri, kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani rais wenu ni mpishi, angahikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote. Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."

Related Posts:

  • Malala asherehekea siku ya kuzaliwa KenyaMshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Malala Yousafzai amezuru kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo atasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Malala alizaliwa 12 Julai 1997 eneo la Mingora, Pakistan katika… Read More
  • Ndege ya kisasa ya Ethiopia yatua KenyaEthiopia imekuwa taifa la kwanza barani Afrika kununua ndege ya kisasa aina ya Airbus A350 XWB. Ndege hiyo, Airbus A350, ndiyo ya hivi karibuni kuzinduliwa na kampuni ya ndege ya Airbus ya Ufaransa. Ndege hiyo, iliyo na uwezo… Read More
  • Boris Johnson alivyokejeli Afrika na watu mashuhuriWaziri mkuu mpya wa Uingereza Theresa May, amemteua Boris Johnson, aliyeongoza kampeni ya taifa hilo kujitoa katika Muungano wa Ulaya kuwa waziri wa mambo ya nje. Johnson, ambaye aliwahi kuwa Meya wa jiji la London amesema Ui… Read More
  • great liabilitiesOne of the great liabilities of history is that all too many people fail to remain awake through great periods of social change. Every society has its protectors of status quo and its fraternities of the indifferent who are n… Read More
  • another way to defeat your enemyAnother way that you love your enemy is this: When the opportunity presents itself for you to defeat your enemy, that is the time which you must not do it. There will come a time, in many instances, when the person who hates … Read More