Je, unapenda kufungua mitandao mbalimbali ya jamii kama Facebook,
Tweeter, Instagram, Google Plus, Snapchat, LinkedIn, Youtube na
mingineyo kila siku?
Kama jibu ni ndiyo, basi uko hatarini kupata tatizo la msongo wa mawazo na wasiwasi.
Utafiti
mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini
Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi
ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya
akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi.
Wakati kukiwa na tatizo hilo, inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana
duniani kote hutembelea mitandao tofauti ya jamii kila siku huku simu za
mikononi zinazowezesha kupatikana mitandao hiyo kirahisi zikizidi
kubuniwa na kuboreshwa.