Recent Posts

PropellerAds

Friday, February 17, 2017

Maharusi waliotumia dola pekee waandaliwa harusi ya kifahari Kenya

Harusi ya marudio ya Wilson na Anne imeandaliwa katika bustani ya kifahari ya Eden Bliss viungani mwa Nairobi
Maharusi waliowasisimua wengi baada ya kutumia Sh100 pekee za Kenya kugharimia harusi, wameandaliwa sherehe ya harusi ya kufana jijini Nairobi.
Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya Eden Bliss, Nairobi ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Wapendanao.
Harusi ya Anne na Wilson Mutura ya awali iligharimu dola moja pekee ya Kimarekani lakini sherehe ya sasa inakadiriwa kwamba imegharimu takriban Sh3.5 milioni (Dola 35,000).
Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya kifahari ya Eden Bliss viungani mwa Nairobi

Pesa hizo zimegharimiwa na makundi mbalimbali yanayohusika katika uandaaji wa sherehe, ambayo yaliungana kwa pamoja na kuchanga pesa kuandalia Anne na Wilson sherehe ya kukata na shoka.
Mmoja wa waandalizi wakuu wa harusi hiyo Aaltonen Jumba kutoka Slique Events Planner Limited, hata hivyo anasema ni vigumu kujua hasa ni kiasi cha peza zilitumiwa kuiandaa.
Ameambia BBC kwamba wahudumu mbalimbali walijitokeza kusaidia kwa kutoa huduma zao, na hakuna pesa taslimu zilizotolewa.
Kuna waliotoa mahema, wengine viti na wengine magari ya kifahari.
Wawili hao wamesafirishwa kwa magari ya kifahari
Kwa sababu walikuwa tayari washafunga ndoa rasmi, kwenye sherehe ya leo, walibadilisha pete zao. Baadhi ya Wakenya mitandaoni wamekuwa wakikosoa uamuzi wa kutumia pesa nyingi kugharimia sherehe nyingine ya harusi kwa wawili hao.
Lakini Bw Jumba anasema wanaokosa sherehe hiyo wamekosa kutambua na kufahamu vyema mambo ambayo yamekuwa yakijiri.
"Wawili hao tayari wamesaidiwa kifedha. Wamepewa shamba la kisasa, wakalipiwa fungate na wameahidiwa pesa za kutumia kama mtaji kuanzisha biashara," alisema.
"Kwa sababu yote yameshughulikiwa, mbona tusiwape kile ambacho walikosa? Kila mtu hutamania sana kuwa na sherehe kubwa ya harusi."

Anne
Wawili hao, wanaoishi eneo la Kasarani, Nairobi, walisifiwa kwa kuonyesha thamani halisi ya mapenzi badala ya kuongozwa na pesa.
Kando na kuandaliwa harusi hiyo, wametunukiwa shamba la kilimo cha kisasa, fungate kwenye hoteli ya kifahari na baada ya sherehe ya leo wanatarajiwa kwenda kwa fungate nyingine mjini Dubai.
Dola yenyewe walioyotumia Anne na Wilson katika harusi yao ya mwanzo waliitumia kununua pete mbili.
Walikuwa wameahirisha harusi yao mara tatu baada ya kukosa fedha za kutosha kuandaa sherehe kubwa ya harusi.
Maombi yao kwa familia na marafiki kuwafanyia mchango, hayakutimizwa.
Baada ya muda, Bwana harusi, Wilson, hakuwa na la kufanya ila kumshawishi mpenzi wake kuhusu uwezo wake.

Related Posts:

  • MAGAZETI YA LEO TZ,APRIL 5 Read More
  • CUF: Hatumtambui Shein kama rais ZanzibarChama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimesema hakimtambui Dkt Mohamed Ali Shein aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi uliopita. Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakizungumza kwa mara y… Read More
  • Bunge kujadili hoja ya kumn'goa Zuma JumanneBunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne. Spika wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Econo… Read More
  • Mwanasiasa wa ANC amtaka rais Zuma kujiuzuluMwanasiasa anayeheshimiwa wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC , Ahmed Kathrada, amejumuika na watu wanaoengezeka, ambao wametoa wito kwa Rais Jacob Zuma ajiuzulu. Siku ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais am… Read More
  • Ndege yagonga gari CaliforniaMtu mmoja ameuawa baada ya ndege moja kuangukia gari alimokuwa kwenye barabara kuu ya California Marekani. Walioshuhudia wanasema kuwa ndege hiyo ilionekana kama iliyokuwa na matatizo ya injini na ikalazimika kutua kwa dharur… Read More