Rais wa Gambia Adama Barrow amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Ousman Badjie.
Jenerali
Badjie alitangaza utiifu wake kwa rais aliyeondoka madarakani Yahya
Jammeh baada ya uchaguzi wa Disemba ulioleta vuta nikuvute.Hata hivyo, chini ya amri yake, jeshi halikutoa msaada wowote pindi vikosi kutoka nchi za Afrika Magharibi vilipoingia nchini Gambia mwezi jana.
Vikosi hivyo vilifanikiwa katika kumshawishi bwana Jammeh kukubali kushindwa na kuondoka nchini.