Meli ya Marekani ya kubeba ndege za
kivita ya USS Carl Vinsion imeanza kile kinatajwa kuwa oparesheni za
kawaida kusini mwa bahari ya China, ikiandamana na meli zingine za
kivita.
Oparesheni hiyo inakuja siku chache baada ya wizara ya
mashauri ya nchi za kigeni ya China kuionya Marekani kwa kupinga uhuru
wa China katika eneo hilo.China inadai kumiliki maeneo kadha ya eneo la bahari ya kusini mwa China.
Imekuwa ikijenga visiwa bandia vilivyo na viwanga vya ndege kwa miaka kadha.
Meli hiyo ya kubeba ndege za kijeshi ilipitia mara ya mwisho eneo la kusini mwa bahari ya China miaka miwili iliyopta, wakati wa mazoezi na jeshi la Malaysia, na imefanya safari 16 kwa miaka 35 ya huduma yake.
Muda mfupi baada ya Donald Trump kuchukua uongozi mwezi Januari, utawala wake uliapa kuizuia China kudhibiti eneo la Kusini mwa bahari ya China.
Siku ya Jumatano msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini China Geng Shuang, aliitaka Marekani kutochukua hatua ambayo itapingauhuru na usalama wa China.