Watu nchini Afrika Kusini
wamegadhabishwa, kufuatia taarifa za mwanamme mmoja, ambaye analaumiwa
kwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyakazi wa shamba, akidhani kuwa mtu
huyo ni ngiri.
Stephen Hepburn alifikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya mauaji.Yeye na mwenzake wa kike walikuwa wakiwawinda ngiri kwenye shamba moja lililo mkoa wa Limpopo kaskazini siku ya Jumamosi, wakati Jan Railo ambaye alikuwa na umri wa miaka 23 aliuawa
Msemaji wa Polisi Motlafela Mojapelo aliiambia BBC kuwa Bwana Hepbaun, alikamatwa siku ya Jumatutu.
Mojapelo aliongeza kusema kuwa bwana Hepburn alisema kuwa aliafyatua risasi eneo ambapo alisikia sauti alipokuwa akiwinda, na alipoenda kuangalia akapata kuwa ni mtu alikuwa amelala chini.
Wanachama wa tawi la chama cha ANC eneo hilo ambao waliofika mahakamani walisema hawaamini ikiwa mauaji hayo yalikuwa ya kimakosa.