Umoja wa Mataifa umeonya kwamba
idadi kubwa ya watoto wanaendelea kuhatarisha maisha yao, kwa kuvuka
bahari ya mediterania kutoka Libya hadi Italia.
Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, linasema watoto 26,000,
wengi wao wakiwa bila walezi, walivuka bahari ya mediterania mwaka jana.Idadi hiyo ni mara dufu ikilinganishwa na mwaka 2015.
Katika ripoti mpya, UNICEF, inasema watoto hao wanadhulumiwa na kunyanyaswa kimapenzi na walanguzi wa binadamu, japo huwa hawatoi ripoti kwa polisi kwa hofu ya kutiwa mbaroni na kurejeshwa Libya.