Hifadhi moja wa wanyama ambayo ni ya
kuwahifadhi tumbili wa barafu imewaua tumbili 57, ambao ilikuwa
ikiwahifadhi baada ya kugundua kuwa nyani hao walikuwa na maumbile ya
kijenetiki ya familia tofauti .
Hifadhi hiyo ya Takagoyama ilichukua hatua hizo baada ya uchunguziwa
DAN kuonyesha kuwa theluthi moja ya tumbili walikuwa na jenetiki ya
familia nyingine ambayo haitambuliwi kuwa ya asilia nchini Japan.Afisa mmoja alisema kuwa tumbili hao walikuwa ili kulinda familia za asili.
Nyani hao waliuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu na msimamizi wa hifadhi akawaandaa maombi kwenye hekalu lililokuwa karibu.