Mgombea wa wadhfa
wa mwenyekiti kutoka Kenya katika tume ya Umoja wa Afrika AU Amina
Mohammed ametaja usaliti miongoni mwa mataifa jirani ya Afrika Mashariki
kuwa sababu ya yeye kutoshinda wadhfa huo.
Balozi Amina ambaye
alipoteza wadhfa huo kwa mpinzani wake kutoka Chad Moussa Faki Mahamat
alilaumu kushindwa kwake kulitokana na uwongo wa majirani za Kenya na
siasa zinazoendelea kati ya mataifa yanayozungumza Kifaransa Francophone
na wale wanaozungumza kizungu Anglophone.Akiongea na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Addis Ababa Amina alisema kuwa alipoteza wadhfa huo kutokana na usaliti wa majirani za Kenya ambao walikuwa wameunga mkono harakati zake.
'Baadhi ya majirani zetu hawakutuunga mkono, walisikika wakizungumzia swala hilo'', Amina alisema bila ya kutaja majina.Nadhani hofu kwamba pengine Kenya ingeshinda ndio iliowafanya kutotuunga
mkono''.
''Nadhani sisi Wakenya ni watu waaminifu sana kwa hivyo ni vigumu kushirikiana na watu wanaohadaa.kwa hivyo nadhani walijiondoa''.
Tukisonga mbele ni funzo zuri kwetu sisi. Katika raundi ya tano ya kura hizo Amina alikuwa anaongoza kwa kura 27 dhidi ya za Mahmat 25'',aliongezea Amina.
Taifa moja halikupiga kura.
Ni wakati huo ambapo mataifa mawili kutoka shirika la IGAD yaliamua kumpigia kura mpinzani wa Amina na hivyobasi kumpatia kura 28 zaidi ya 26 zilizohitajika ili mgombea kuibuka mshindi.